EU kuwawekea vikwazo Warusi sita kuhusu kupewa sumu Navalny

 


Umoja wa Ulaya na Uingereza zimetangaza leo vikwazo dhidi ya raia sita wa Urusi, baadhi wakiwa ni maafisa wa ngazi za juu nchini humo, na shirika moja, kuhusu tukio la kupewa sumu kiongozi wa upinzani Urusi Alexei Navalvy. 


Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Heiko Maas, ambayo ndiyo inayoshikilia kiti cha kupokezana cha urais wa Umoja wa Ulaya amesema ni kupitia tu msimamo wa wazi na kwa kuzingatia kanuni ambapo Umoja wa Ulaya utapiga hatua kuhusiana na Urusi. 


Vikwazo hivyo ni pamoja na marufuku ya kusafiri katika Umoja wa Ulaya na kuzuiwa mali za watu na shirika linalolengwa. Orodha hiyo inawajumuisha Alexander Bortinikov, mkuu wa shirika la usalama wa taifa na Sergei Kiriyenko, naibu mkuu wa utumishi wa serikali. 


Umoja wa Ulaya pia umeilenga Taasisi ya Utafiti wa Kisayansi ya Kemia ya Kikaboni na Teknolojia. Uingereza imesema pia itatekeleza vikwazo hivyo vya Ulaya na itaviendeleza mara baada ya kujiondoa kwenye kipindi cha baada ya mchakato wa Brexit mwishoni mwa mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments