Na Faruku Ngonyani ,Mtwara
Halmashauri ya wilaya ya Mtwara iliyopo Mkoani Mtwara imekabidhi vitambulisho vya bima ya afya iliyoboreshwa (ICHF) kwa Wazee wasiojiweza 395 wa kata ya Nanguruwe.
Awali, akiongea na wazee hao, Mgeni Rasmi Wakili Msomi Arthur Mbena amesema kuwa utaratibu huo ni sehemu ya Mpango wa Bajeti ya Halmashauri ambapo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 imeadhimia kugawa vitambulisho vipatavyo 995 kwa wazee wasiojiweza ikiwa ni sehemu ya kuwaboreshea kupata huduma ya Afya ndani ya Halmashauri hiyo.
Lakini pia Halmashauri hiyo imrendelea kutoa elimu juu ya huduma Mabalimbali kwa wazee ikiwemo Msamaha wa Matibu kwa wazee wasiojiweza wenye umri wa Miaka 60, lishe, na ustawi wa Jamii.
Aidha Halmashauri hiyo imetoa fursa kwa wazee hao kuwa katika vituo vya kutolea huduma za Afya afya kumeanzishwa Dirisha maalumu la Wazee kwaajili ya kushughulikia kero na malalamiko Yao na ni vyema wakalitumia ili kwaweze kuafanyiwa maboresho Zaidi haswa kwenye eneo hilo la Afya.
.
