Polisi yawakamata washukiwa 44 kwa unyanyasaji wa watoto



Polisi huko Sydney wakimkamata mwanaume mmoja anayeshukiw a kutengengeza video za unyanyasaji wa watotoImage caption: Polisi huko Sydney wakimkamata mwanaume mmoja anayeshukiw a kutengengeza video za unyanyasaji wa watoto

Polisi huko Australia imewakamata wanaume 44 nchini humo wanaoshukiwa kutengeneza na kumiliki video za kunyanyasaji watoto.


Watoto 16 wameokolewa, kwa mujibu wa Polisi nchini Australia.


Kamata kamata hiyo imefuatia uchunguzi uliofanywa kwa muda mrefu wa picha na video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.


Kukamatwa kwa washukiwa kati ya umri wa miaka 19 na 57 kumefanyika katika kila jimbo la Australia.


Polisi walifungua mashtaka karibu 350 yote yakiwa yanahusishwa na umiliki na utengenezaji wa video za kunyanyasa watoto.


Washukiwa walifanyakazi katika viwanda mbalimbali ikiwemo majengo, usafirishaji, utekelezaji wa sheria na kwenye mahoteli.



Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi