Hofu ya bomu ndani ya behewa la treni Ujerumani


Bomu lililokuwa limetegwa kwenye behewa la treni mjini Köln nchini Ujerumani, limeripotiwa kuteguliwa.


Hofu hiyo ya bomu imepelekea polisi wa kukabiliana na ugaidi kuanza harakati za kiusalama.


Kulingana na maelezo yaliyotolewa na idara ya polisi, iliarifiwa kupatikana kwa bomu lililokuwa limetegwa ndani ya sanduku baada ya kugundulika na wahudumu wa usafi usiku wa Ijumaa kwenye kituo cha Köln-Deutzerfeld.


Polisi walifunga utepe wa usalama eneo lile, na kuanzisha shughuli ya ukaguzi kwa msaada wa mbwa wa ulinzi, kwa kuhofia uwezekano wa kuwepo kwa bomu lingine ndani ya behewa.


Baada ya kupatikana kwa bomu hilo moja, liliteguliwa na vikosi husika vya polisi na kuimarisha hali ya usalama.  


Wakati huo huo, treni nyingine 27 zilizokuwa zimeegeshwa kituoni pia ziliweza kufanyiwa ukaguzi wa mabomu ili kuhakikisha zipo salama.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi