Kamanda wa Polisi viwanja vya ndege Tanzania awataka madereva bodaboda, taxi na bajaji kuimarisha ulinzi


 Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege Tanzania ACP. Jeremia Shilla leo Oktoba 26 amezungumza na madereva wa bodaboda zaidi ya 50, madereva bajaji na madereva taxi wa kituo cha njia panda Airport kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama katika eneo hilo hasa kwa wageni ambao wanaingia nchini kwa kutumia uwanja huo wa ndege.

Kamanda Shilla amewapongeza kwa kuitikia wito wake ambapo amewaeleza kuwa katika utendaji wao wa kazi wanatakiwa kuwa na huduma bora kwa mteja ikiwa ni pamoja na kuwafikisha salama maeneo wanayokwenda hasa wageni wanaotua katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na si kuwafanyia vitendo vya kihalifu kama uporaji na unyang'anyi.


Pia amewataka madereva hao kuwa na ushirikiano na Jeshi la polisi Viwanja vya ndege kwa kutoa taarifa za matukio ya kihalifu hasa wanapomuona mtu wasiyemfahamu miongoni mwao katika maeneo hayo.

Aidha aliwasisitiza kuwa wajitahidi kuwa na vitambulisho pamoja na reflekta zitakazokuwa zinawapa utambulisho kwa abiria wao hasa raia wa kigeni

Post a Comment

0 Comments