Maganja wa NCCR: Nipeni kura nisuke nchi


Na Timothy Itembe,  Mara.

Mgombea urais kupitia Chama cha NCCR Mageuzi jana alipokuwa katika mkutano wa kampeni ndani ya jimbo la Tarime mjini amejinadi kwa kuomba kura kwa kutoa ahadi lukuki .

Jeremia Kulwa Maganja alisema kuwa akipatiwa ridhaa na wapiga kura ataenda kubadilisha sheria zinazoonekana kuwa kandamizi ustawi kwa wananchi huku akiboresha  uchumi wa Taifa na kutengeneza  mazingira rafiki kwa mfanyabiashara.

Mganja aliongeza kuwa akiwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania  atahakikisha anaimarisha muungano wa Tanzania na Zanziba na kuondoa kero ndogo ndogo zinazokwamisha kufikia maendeleo ndani ya muungano huo huku baadhi ya sheria na taratibu zikiugawa muungano.

“Mimi mkinipa ridhaa ya kuwa Rais nitasimamia mchakato wa katiba mpya ya Jaji Sinde Waryoba ambayo itashirikisha wananchi kutoa maoni ili kukamilika na kutumika,nitasimamia kuboresha elimu na miundombinu yake ili wanafunzi wakapate  elimu bora pia  nitaenda kufuta michango iliyokero kwa wazazi na walezi na wanafunzi wanasoma bure msingi hadi chuo,nitahakikisha walimu wanaenda semina za mara kwa mara kulikabiliana na mitaala ya kisayansi kadiri inavyokuja,nitakikisha ninaboresha uchumi wa Taifa hili ili kila mfanyabiashara na mtanzania kunufaika na rasilimali zilizopo”alisema Maganja. 

Katika Afya Mganja alisema kuwa akifanikiwa na kuwa rais ataenda kufuta vitambulisho vya Bima ya Afya kwasababu amegundua kuwa wengi walio na kadi ya vitambulisho hivyo hawanufaiki na matibabu badala yake waambiwa kwenda kunua dawa madukani ama wanaabima bima hizo zinazolenga hospitali ya eneo moja  huku bima hizo zikibagua baadhi ya magonjwa ya kutibu.


Naye mgombea ubunge wa NCCR Mageuzi jimbo la Tarime mjini,Mery Nyagabona alisema kuwa akipewa ridhaa ya kuwa mbunge atajenga hoja ya kujenga Soko ambalo limebomolewa ili wafanyabiashara waende kufanya biashara upya na kukuza mitaji na uchumi wa halmashauri.

Nyagabona aliongeza kusema kuwa amejitokeza kugombea nafasi hiyo kwasababu wagombea wa vyama vilivyopo Chadema na CCM wameshindwa kuwaletea wananchi maendeleo ambapo alisema kuwa akipewa ridhaa atahakikisha anawasemea bungeni na jimbo lake kupata maji safi na salama badala ya wananchi kutumia  maji yenye rangi kama chai ya storonki (Chai ya rangi).

Kwa upande wake Naibu katibu mkuu Vijana Taifa,Ndihaloye Kifu aliwataka wananchi kuwachagua wagombea wa Chama chake badala ya  kuchagua wagombea wa CCM kwasababu wameshindwa kuwaleta wananchi maendeleo.

Kiongozi huyo aliwataka wapiga kura kuacha siasa za ushabiki ambazo zimekwamisha maendeleo kwa mda mrefu badala yake wachague viongozi wenye maono ambao watawaletea maendeleo.

Kiongozi huyo aliomba chama chake kama kikishika kikifanikiwa kuingia ikulu kiende kubadilisha mfumo wa elimu uliopo wa vijana kusoma huku wakitegemea  kuajiriwa badala yake wanafunzi wafundishwe elimu ya kujiajiri pindi wanapokuwa wamehitimu.


 

Post a Comment

0 Comments