Mama Samia aahidi kuboresha huduma za afya na kutatua changamoto za mama wajawazito

 


Na, Baraka Messa, Momba.

MGOMBEA mwenza Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Jimbo la Momba mkaoani Songwe kuendelea kukiamini chama  hicho ili waweze kutatuliwa changamoto yamiundo mbinu ya barabara na madaraja ambayo hupelekea akinamama wajawazito kujifungulia nyumbani. 

Mgombea mwenza alisema hayo hivi karibuni katika kata ya Chitete wilayani Momba akiwa kwenye Kampeni za kumnadi mgombea Urais, Wabunge na Madiwani mkoani Songwe ambapo alieleza mikakati ya Serikali ya awamu ya tano kuwa ni kuhakikisha wanaboresha sekta ya afya kwa kuboresha miundo ya barabara na madaraja ambavyo huunganisha vijiji na kata ambako huduma za afya hupatikana.

Alisema kuwa anatambua kuwa miundo mbinu ya usafirishaji kwa Jimbo la Momba inachangamoto kubwa Hali ambayo husababisha wananchi wa eneo Hilo kukosa huduma za kijamii hasa akina mama wajawazito kushindwa kusafir kujifungulia  hospitalin.

"Mpango wa Serikali ni kuhakikisha kila Kijiji kinakuwa na Zahati na kilakata inakuwa na kituo Cha afya , tayari tulishaanza tupeni miaka mitano mingine ndani ya miaka mitatu tuhakikisha tunamalizia na kutatua changamoto ya wajawazito kutembea umbali mrefu kufuata matibabu tofaut na Sasa ambapo kumekuwa kukiripotiwa changamoto nyingi na kupelekea wengi kushindwa kuhudhuria klininiki na kujifungulia njiani " alisema 

Aliongeza kuwa pia wanatambua kuwa Licha ya Mito mingi inayozunguka Jimbo la Momba kunachangamoto kubwa ya upatikanaji wa maji na kupelekea wananchi kukosa maji Safi na salama.

Kuhusu Elimu Samia alisema ndani ya miaka mitano uandikishwaji watoto kuingia darasa la Kwanza imeongezeka na kupelekea idadi ya watoto wanaotoka kaya masikini kuongezeka ukilinganisha na miaka ya nyuma.

Kwa upande wake Mgombea Ubunge Jimbo la Momba Condester Sichalwe alisema kukatika kwa vivuko na madaraja kipindi Cha masika hupelekea kuvunjika kwa Mawasiliano miongoni mwa vijiji na kata kukatika na kupelekea baadhi ya akina mama kujifungulia njiani.

"Tunaomba kuboreshewa na kuongezewa zahanati na vituo vya, kama ulivyo ona miundo mbinu ya Jimbo letu ilivyo na shida hivyo pamoja na kazi kubwa ambayo Serikali imetusaidia tunaendelea kuiomba Serikali yetu sikivu kutuboreshea zaidi " alisema Condester.

Alisema Jimbo la Momba Lina kata 12 na Vijiji 72 , ambavyo vyote pamoja na changamoto zake anazijua hivyo aliwaomba wananchi wa Momba kumuunga mkono na chama Cha mapinduzi ili waweze kupata maendeleo na kukuza uchumi wao.

Post a Comment

0 Comments