https://monetag.com/?ref_id=TTIb Sisi ni binadamu kama nyie saa nyingine tunapitiwa- Shamsa Ford | Muungwana BLOG

Sisi ni binadamu kama nyie saa nyingine tunapitiwa- Shamsa Ford

 


Msanii wa filamu na mfanyabiashara wa mavazi, Shamsa Ford ameachia ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuwataka mashabiki wasipende kuwahukumu watu maarufu kwa makosa yao kwani nao ni binaadam wanapitiwa kama inavyotokea kwa watu wengine.

Shamsa amesema kuna watu wakiwaona mastaa mitandaoni wanahisi ni tofauti na walivyo wao ndiyo maana wanawakuhumiwa  kwa kuwashambulia na matusi pale wanapokosea.

"Wengine wakituona kwenye mitandao wanatuhukumu tofauti, sisi ni binadamu kama nyie saa nyingine tunapitiwa kama binadamu wengine kwasababu hakuna mwanadamu aliyekamilika zaidi ya  Mungu ila maisha yetu pia huwa tunaishi kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu, tusijisahau sana na dunia".

"Kulikuwa na matajiri wengi, wazuri wengi, watu maarufu wengi lakini leo hii hatupo nao duniani, tuishi kwa kuthaminiana epuka kumuumiza mwanadamu mwenzio kwa makusudi sisi sote si chochote mbele ya Mwenyezi Mungu" ameeleza @shamsaford

Aidha, msanii huyo amesema amekaa kimya na kudhalilishwa vya kutosha hivyo atatangaza siku ya kuwa na mkutano na waandishi wa habari ili kuzungumzia ukweli wote yanaondelea dhidi yake.

Post a Comment

0 Comments