Uongozi wa amani ya mkoa wa pwani yaomba dua maalumu kuombea uchaguzi


NA VICTOR MASANGU PWANI

KAMATI i ya amani ya Mkoa wa Pwani pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wamekutana kwa ajili ya kufanya dua maalumu la kuliombea Taifa pamoja na kuweza  kupanga mikakati kabambe ambayo itasaidia katika  kudhibiti hali ya  machafuko na uvunifu wa amani katika kuelekea uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Octoba 28 mwaka huu.

Akizungumz ana waandishi wa habari katika kikao hicho Mwenyekiti wa Kamati ya amani ya Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amesema kwamba   lengo kubwa  kwa sasa ni kusimamia suala la amani na utulivu ili kuweza kuwapa fursa wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la upigaji a kura.

Aidha Ndikilo aliwatoa  hofu wananchi wa Mkoa wa Pwani na kuwataka wale wote waliojiandikisha kutoogopa  vitisho vya baadhi wa wagombea kwa kutoa lugha za matusi  na badala yake wajitoikeza kwa wingi katika kupiga kura na kuwahimiza  viongozi wote wa  dini kuendelea kufanya maombi  usiku na mchana katika kipindi chote cha  kuelekea uchaguzi mkuu.

Kwa upande wake Shekh wa Mkoa wa Pwani Hamisi Mtupa alisema  wao kama viongozi wa dini watahakikisha wanaliombea Taifa katika kipindi chote cha kuelekea uchagzui Mkuu na kuliomba jeshi la polisi juhakikisha kwamba linaimarisha hali ya ulinzi na usalama ili kuepukana na machafuko na kudhibiti kuibuka kwa vurugu zozote.

 Aidha Ndikilo alitoa rai kwa viongozi wa dini kuwashirikisha waumini wao kwenye nyumba za ibada kuliombea Taifa kuelekea siku ya kupiga kura ikafanyike kwa utulivu na amani.

Alisema, Mkoa huo umekamilisha maandalizi yote kwa ajili ya kupiga kura siku ya Octoba 28 na yote hayo hayawezi kufanyika bila huruma ya Mungu.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema,  ni jukumu la  viongozi wa dini kuzidisha maombi kuomba amani ili kura zipigwe kwa amani na utulivu  na mshindi atangazwe bila shinikizo.

Alisema, Serikali inahakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu, na kwamba Mkoa huo unatarajia baada ya kupiga kura zihesabiwe kwa utulivu na mshindi kutangazwa bila kikwazo ili mkoa huo uendelee kubaki na hali ya amani baada ya Uchaguzi.

Aliwasisitiza wananchi wenye sifa kujitokeza kupiga kura kujitokeza kutimiza wajibu wao na kuzingatia kikamilifu maelekezo kutoka tume ya Uchaguzi.

Mwenyekiti Mwenza wa kamati ya amani ya Mkoa wa Pwani Hamis Mtupa alisema kipindi chote cha Kampeni hapakuwa na uvunjifu wa amanina hivyo kuwaomba wananchi kuendeleza amani siku ya Uchaguzi.

Alisisitiza wananchi kurudi nyumbani baada ya kupiga kura, huku akitoa tahadhari kwa Jeshi la polisi kuhusiana na mkesha wa maulidi ambao utakuwa siku ya kupiga kura.

Naye Padri Benno Kikudo alisema wanaendelea na maombi kuiombea nchi kufanya uchaguzi kwa amani huku akiwasihi wagombea kuwa tayari kupokea matokeo baada ya kura kupigwa.

Ahmad Seif mmoja wa wajumbe wa kamati ya amani aliiomba Serikali kuwezeaha kamati hiyo ya mkoa kufika maeneo ya shule kuwaelimisha Vijana umuhimu wa kulinda amani.

Post a Comment

0 Comments