Oct 17, 2020

Wanafunzi Makurunge kujengewa shule kuondokana na kwenda mbali kufuata masomo

  Muungwana Blog 3       Oct 17, 2020


Na Omary Mngindo, Makurunge

WANAFUNZI wanaosoma Sekondari kutoka Vijiji vinavyounda Kata ya Makurunge Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wanataraji kuondokana na adha ya kwenda umbali mrefu kufuata masomo.

Hatua hiyo inayolenga kuwaondolea usumbufu wanafunzi hao sanjali na gharama ya nauli za kwenda na kurudi kila siku kwa wazazi na walezi wao, pia itakuwa suruhisho kwa walengwa hao ambao kila siku wanalazimika kutumia nauli zaidi ya shilingi 3,000.

Matumaini hayo yametolewa na Mgombea Udiwani katani hapo Hamisi Mbonde, akizungumza na wana-Makurunge katika mkutano wa Kampeni mbele ya mgombea Ubunge jumbo la Bagamoyo Muharami Mkenge aliyeambatana na Menaja wake wa Kampeni Yahya Msonde.

Mbonde alisema kwamba hatua hiyo imefuatia juhudi kubwa za wazazi, walezi na wadau mbalimbali waliojitolea kwa hali na mali katika kufanikisha upatikanaji wa matofali zaidi ya elfu saba, yanayotaraji kuanza kutumika kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari katani hapo.

"Mheshimiwa mgombea Ubunge pamoja na Meneja wa Kampeni nawajulisha kwamba wananchi wa Vijiji vinavyounda Kata ya Makurunge tumechangishana matofari zaidi ya 7,000, tunachosubiri ni ujio wa wataalamu wa majengo kutoka halmashauri ili ujenzi uanze," alisema Mbonde," alisema Mbonde.

Kwa upande wake Meneja wa Kampeni Msonde alisema hiyo ni hatua kubwa iliyofikiwa na wananchi hao, kwano inakwenda kuwaondolea changamoto wanafunzi wanaosafiri umbali mrefu kwenda kusoma, pia kuwapunguzia gharama za nauli wazazi na walezi wao.

"Hii ni hatua kubwa na inaonesha wana-Makurunge mmedhamilia kwa kutuma nguvu zenu kupambana naa changamoto zinazowakabili, hongereni sana Oktoba 28 tukiwachagua wagombea wanaotokea Cham Cha Mapinduzi CCM watakuja kuwaongezea nguvu," alisema Msondr.

Akizungumza na wananchi hao, Mkenge alisema kuwa Serikali imejiwekea utaratibu wa kuunga mkono nguvu za wananchi wanaoibua miradi, kisha kuanza itekelezaji wake ambapo serikali kupitia halmashauri au Serikali Kuu kuunga mkono juhudi husika.

"Mmefanya juhudi kubwa za kuhakikisha mnawakomboa vijana wetu waliokuwa wanasafiri kutoka Makurunge na vitongoji vyake kwenda Fukayosi au Hassanal Damji Bagamoyo eneo la Magomeni ambao kuanzia mwakani kama alivyosema mgombea udiwani ndigu yangu Mbonde kwamba wataanza kusoma hapa hapa," alimalizia Mkenge.

logoblog

Thanks for reading Wanafunzi Makurunge kujengewa shule kuondokana na kwenda mbali kufuata masomo

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment