Waziri mkuu wa Thailand ataka maandamano yakomeshwe

 

Waziri Mkuu wa Thailand Prayut Chan-O-Cha amesema leo kuwa nchi hiyo inapaswa kudhibiti kile alichotaja kuwa "maandamano haramu" yanayoendeshwa na vuguvugu la kudai demokrasia dhidi ya utawala wake. 

Akihutubia kikao maalamu cha bunge kilichoitishwa kujadili namna ya kumaliza wimbi la maandamano ya miezi kadhaa , Chan-O-Cha amesema licha ya raia kuwa na haki ya kuandamana, vyombo vya usalama vina wajibu wa kukomesha maandamano haramu.

 Katika wiki za hivi karibuni, Chan-O-Cha, mkuu wa zamani wa jeshi aliyeongoza mapindunzi mwaka 2014, amekabiliwa na shinikizo kutoka kwa maelfu ya waandamnaji wanaomtaka kujiuzulu. Maandamano hayo yanayoongozwa na wanafunzi pia yanataka kuandikwa katiba mpya, kukomesha ukandamizaji wa serikali na kuufanyia mageuzi mfumo wa kifalme wa nchi hiyo.

Post a Comment

0 Comments