Oct 24, 2020

Waziri wa Ulinzi wa Uturuki akutana na Waziri mwenzie wa Indonesia


Waziri wa Ulinzi wa Kitaifa Hulusi Akar alikutana na Waziri wa Ulinzi wa Indonesia Prabowo Subianto.

Kulingana na taarifa kutoka kwa Wizara ya Ulinzi, iliarifiwa kuwa Subianto alikuwa amekuja Uturuki kufuatia mwaliko rasmi, na kupokewa kwa gwaride la heshima lililoandaliwa na jeshi.

Baada ya kumaliza mazungumzo ya ana kwa ana,  Akar na Subianto waliongoza mkutano baina ya wajumbe kutoka pande zote.

Kwenye mikutano hiyo ya mazungumzo, viongozi walitoa maoni na kubadilishana mawazo  juu ya maswala ya ulinzi na usalama wa pande mbili na wa kikanda, na kuweka ushirikiano katika sekta ya ulinzi.


KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger