F Darasa lisilo pata daraja la 4 na 0 UMAWANJO waahidi kutikisa 2020 | Muungwana BLOG

Darasa lisilo pata daraja la 4 na 0 UMAWANJO waahidi kutikisa 2020


Na Amiri Kilagalila, Njombe.

Wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Umawanjo mkoani Njombe wameahidi ufaulu wa kiwango cha juu katika matokeo yao mara baada ya kumaliza mtihani wao wa kuhitimu kidato cha nne.

Darasa hilo lenye jumla ya wanafunzi 72 wanaotarajia kuanza mtihani wao karibuni katika shule ya sekondari Umawanjo inayomilikiwa na umoja wa mapadre wazalendo wa kanisa la Romani Katoriki mkoani Njombe.Wamesema matarajio yao ni makubwa katika mtihani wao kutokana na juhudi za makusudi zilizofanywa kwa pamoja na walimu katika ujenzi wa taaluma ya darasa hilo kwa kutokupata daraja la nne na 0 tangu walipoanza 2017.

Evaristo Mangula na Stanley Hongoli ni miongoni mwa wanafunzi wa darasa hilo katika shule hiyo ya wavulana iliyopo kata ya Lugarawa wilayani Ludewa,kwa niaba ya Kidato cha nne wamesema matarajio yao ni makubwa kutokana na jinsi walivyojipanga kwa miaka minne huku wakishukuru Jimbo katoriki la Njombe,wazazi,shule na walimu kwa kufanikiwa kujenga umoja,mshikamano na taaluma katika shule hiyo.

"Tumefanikiwa kufanya vizuri kitaaluma tangu kuanzishwa kwa shule,kwani hatujawahi kupata daraja la nne na sifuri.tunatoa shukrani za dhati kwa baba askofu wa jimbo katoriki la Njombe Alfred Maluma na mapandre wote wa jimbo katoriki la Njombe pia kwa walimu wote kwa kazi kubwa wanayoifanya pamoja na wazazi na walezi kwa michngo yao kwa kuwa hakika hawakukosea kutuleta hapa"alisema Evaristo Mangula

Stanley Hongoli alisema "Kidato cha nne tunaahidi kuwa tutafanya vizuri katika mtihani wetu wa taifa kwa ufaulu wa mtu mmoja mmoja,ngazi ya shule,wilaya,mkoa na hata kitaifa ili kuipandisha shule kitaifa tukishirikiana na walimu katika kupandisha ufaulu huo wa shule"

Baadhi ya wazazi walioshiriki mahafali ya wanafunzi hao wametoa wito kwa watoto wao kuongeza nguzu watakapohitimu kidato cha nne  ili kufanikiwa katika ngazi nyingine ya kielimu.

Edward Wayutile ni afisa tarafa wa tarafa ya Liganga kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Ludewa Adrea Tsere na mbunge mteule wa jimbo la Ludewa wakili Joseph Kamonga.Amepongeza ufaulu shule hiyo kwa kuongeza kiwango cha ufulu pamoja na uboreshaji wa mazingira ya shule.

"Nipongeze uongozi wa shule kwa kuboresha mazingira ya shule pamoja na kuongeza kiwango cha ufaulu  na kumbu kumbu zangu kidato cha nne mwaka 2018 waliopata daraja la 1 walikuwa 14 lakini 2019 daraja la 1 ni 35"alisema wayutile

Alexander Mlelwa na pandre wa parokia ya Lugarawa na mkurugenzi wa shule hiyo ametoa wito kwa wanafunzi hao kuwa mabarozi wa shule hiyo huku akiahidi shilingi laki moja kwa kila mwanafunzi atakayepata daraja la kwanza.

"Kauli yetu ni elimu na malezi bora na hii lazima tuilinde kwa ghalama yeyote na sasa wanafunzi mnamaliza mkaipeperushe vizuri bendera ya umawanjo na mkajiheshimu mnakoenda"alisema Alexander Mlelwa

Shule hiyo inayofikia kidato cha nne kwa mara ya sita ina jumla ya wanafunzi 289,kidato cha kwanza wakiw 80,kidato cha pili 76,kidato cha tatu 58 huku kidato cha nne waliosajiliwa kufanya mtihani wa taifa ni 73 huku mmoja akiwa ni mtoro wa kudumu na kubakia wanafunzi 72.

Aidha shule hiyo imefanikiwa kufanya vizuri katika majaribio na mitihani mbali mbali kwa ngazi tofauti na kufanikiwa kitaluma huku ikiwezesha kupata matokeo mazuri mfano wa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2019 uliowezesha wanafunzi kupata daraja la kwanza wanafunzi 35,daraja la pili wanafunzi 22,daraja la tatu hakuna la nne hakuna na sifuri hakuna huku wanafunzi waliofanya mtihani wakiwa 57.

 

Post a Comment

0 Comments