Kampuni ya DOT yatakiwa kulipa nusu ya fedha wanazodaiwa na TRA ili waweze kufunguliwe akaunti zao za kibenki


 

Na Faruku Ngonyani, Mtwara.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa ametoa siku moja kwa kampuni ya DOT inayojenga barabara ya Mtwara - Mnivata kwa kiwango cha lami kulipa nusu ya pesa wanaidaiwa na TRA ,ambapo  kampuni hiyo inadaiwa Zaidi ya milioni mia tatu ya makato ya mishahara ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa kufikia siku ya kesho tarehe 21 Novemba 2020 saa sita mchana Dot anapaswa kuandika barua ya kuonyesha analipa nusu ya  Milioni mia tatu tisini na moja  pesa hiyo iwe imelipwa TRA ili waweze kufunguliwa akaunti zao za kibank na hatimae kulipa mishara ya wafanyakazi wao.

Hayo yamefikiwa mara baada ya wafanyakazi wa kampuni hiyo kudai mishara ya miezi miwili mfululizo.

Awali Kampuni ya DOT ilieleza kuwa wameshindwa kulipa mishara ya wafanyakazi kwa kuwa account zao zimefungwa na TRA na wanashindwa kutoa fedha hizo na kuwalipa wafanyakazi wao.

Kwa upande wa mkurugenzi wa kampuni hiyo ya DOT ameahidi kulipa kiasi hiko cha fedha kabla ya muda ambao Mku wa Mkoa aliotuo.


Kampuni ya DOT imepata kandarasi ya ujenzi wa barabara kutoka Mtwara mpaka Kijiji cha Mnivata kwa kiwango cha lami.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items