Kiongozi wa Thailand aamuru ukandamizaji dhidi ya maandamano


Waziri Mkuu wa Thailand Prayut Chan-o-cha ameziamuru idara za usalama leo kuwakabili waandamanaji wanaodai demokrasia, siku chache baada ya polisi kutumia mabomu ya kutoa machozi na mizinga ya maji kuyavunja maandamanao mjini Bangkok. 

Prayut, aliyeingia madarakani katika mapinduzi ya mwaka wa 2014, ametoa taarifa hiyo leo akiwaonya waandamanaji kuwa watakabiliwa na nguvu kubwa za kisheria. 

Amesema serikali na idara za usalama zinahitaji kuimarisha mbinu zao na kutekeleza vipengele vyote vya sheria. Thailand tangu Julai imekumbwa na maandamano yanayoongozwa na vijana wanaodai katiba mpya, miito isiyo ya kawaida ya kuufanyia mageuzi ufalme wa nchi hiyo, na kumtaka Prayut ajiuzulu. 

Makabaliano nje ya bunge ya siku ya Jumanne kati ya waandamanaji wanaounga mkono demokrasia na wanaouunga mkono ufalme yalisababisha ghasia, ambapo watu sita walipigwa risasi.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items