Loading...

Nov 21, 2020

Makombora ya roketi yawauwa watu 8 Kabul


Idadi ya waliokufa kutokana na shambulizi la roketi lililoulenga mji mkuu wa Afghanistan, Kabul mapema leo hii imeongezeka na kufikia watu wanane. Maafisa nchini humo wamethibitisha vifo hivyo kwa kusema na watu wengine 31 wamejeruhiwa. 


Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani, Tariq Arian pamoja na kulinyooshea kidole kundi la Taliban kuhusika na maafa hayo amesema magaidi walifyatua makombora 23 katika mji wa Kabul. Vyanzo vya kipolisi pia vimethibitisha vifo hivyo.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger