Miaka 3 baada ya kuondolewa Mugabe, matumaini yatoweka Zimbabwe


Leo hii imetimia miaka mitatu kamili tangu kuondolewa madarakani aliyekuwa rais wa Zimambwe, hayati Robert Mugabe. Kiongozi huyo alijiuzulu Novemba 21, 2017, akihitimisha karibu miongo minne ya utawala wake wa kiimla. 


Kujiuzulu kwake kulifanyika siku kadhaa baada ya vifaru vya kijeshi kupiga doria katika jiji la Harare. 


Mapinduzi dhidi ya Mugabe yalikaribishwa kwa shangwe na maelfu ya watu walimiminika barabarani kusherehekea hatua hiyo. 


Lakini wadadisi wanasema leo hii, miaka mitatu baada ya mrithi wake Emmerson Mnangagwa kuchukua madaraka matumaini makubwa ya mabadiliko yameingia katika hali isiyoeleweka kabisa. 


Ibbo Mandaza, kiongozi wa asasi zinazojihusisha na siasa na uchumi wa upande wa kusini mwa Afrika amesema hakuna kilichobadilika, na mambo yameendelea kuwa mabaya zaidi. Amesema viwango vya umasikini na ukandamizaji vimeongezeka zaidi.

Post a Comment

0 Comments