Ndugai:Nitawatendea haki wote


Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai amesema iwapo atachaguliwa kuwa Spika wa Bunge la 12 atatenda haki kwa wabunge wote na kulifanya bunge hilo kuwa la mfano.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo Jumanne Novemba 10, wakati akiomba kura za kuwa Spika wa Bunge la 12 lilioanza leo jijini Dodoma.

Aidha, amesema kuwa iwapo atapata nafasi hiyo kwa mara nyingine, bunge hilo litakuwa la mfano huku akiahidi kutenda haki kwa wapinzani ikiwamo kuwalinda kwa manufaa ya Watanzania.

Zoezi la uchaguzi wa Spika linaendelea ambapo wabunge 263 wanashiriki uchaguzi huo.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi