Tetesi za soka kimataifa

 

Kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba anasema kwa sasa anapitia kipindi kigumu sana cha kazi yake ya soka kutokana na muda wake wa mchezo katika Old Trafford. (RTL via Goal)

Kiungo wa kati wa AC Milan Mturuki Hakan Calhanoglu, 26, huenda yuko njiani kuelekea Atletico Madrid baada ya mazungumzo ya mkataba na klabu hiyo ya Italia kukumbwana tatizo, ingawa Manchester United bado wanamtaka (Mundo Deportivo)

Chelsea tayari wamekwisha kubali mkataba wa kumuuza midifilda wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 26, kwa Napoli wakati uhamisho wake wa mkopo utakapomalizika mwishoni mwa msimu . (Gazetta Dello Sport via Teamtalk)

Manchester City wanasaini mkataba na mshambuliaji ambaye ni kipaumbee chao cha mwaka 2021, nyota wa Borussia Dortmund Mnorway Erling Haaland, 20, na kiungo wa mbele wa Inter Milan Muargentina Lautaro Martinez, 23, ambao ndiye wachezaji wanaowalenga zaidi . (90min)

Mchezaji wa safu ya ulinzi ya Chelsea Mjerumani Antonio Rudiger, 27,yuko makini kuhusu kujiunga na klabu ya Barcelona wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa mwezi Januari baada ya kutopendelewa katika Stamford Bridge. (Sport via Metro)

Mkurugenzi wa mchezo wa Liverpool Michael Edwards ameripotiwa kuamua dhidi ya kumuhamisha mlinzi wa Napoli Msenegal Kalidou Koulibaly, 29msimu huu kwasababu ya pesa anazotaka alipwe . (Daily Star)

Mkufunzi wa zamani wa RB Leipzig Ralf Rangnick anaamini kuwa kiungo wa safu ya kati-nyuma Dayot Upamecano, 22, ambaye Liverpool wanamlenga kumchukua, anaweza kuleta mafanikio katika Bayern Munich. (Goal)

Juventus wako tayari kumnunua nyota mchanga anayechezea Ajax Ryan Gravenberch lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Barcelona katika kumsaini kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 18 tu . (Tuttosport - in Italian)

Post a Comment

0 Comments