Timu 92 kutoka Tanga, Bagamoyo na Zanzibar kuwania Milioni 5 za Dully Cup


Na Omary Mngindo, Bagamoyo

TIMU 92 zinazochuana katika miji ya Bagamoyo, Tanga na Visiwani Pemba kuwania kitita cha shilingi milioni 5 zitazotolewa na Mdhamini wa michuano hiyo Abdul Salum.

Michuano hiyo inayolenga kuibua na kuendeleza vipaji kwa vijana, kwa hapa Bagamoyo yanatimua vumbi mwenye uwanja mkongwe wa Mwanakalenge ambapo vilabu,, vinashiriki kinyang'anyiro hicho.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini hapa, Salumu alisema kuwa michuano hiyo iliyoanza mwaka 2016 imekuwa ikichezwa katika mji wa Pemba pekee, lakini mwaka huu ameongeza vituo vya Bagamoyo na Tanga.

"Bingwa katika kila kituo kutoka Bagamoyo na Tanga watakwenda Visiwani Pemba kucheza na bingwa wa huko, ambako ndiko atakapopatikana bingwa wa Dully Cup atayejinyakulia kitita hicho," alisema Salumu.

Aliongeza kuwa kituo cha Pemba kina timu 48, Tanga 32 wakati Bagamoyo kuna timu 12 ambapo alisema kwamba kituo cha Bagamoyo bado hamasa ya mashabiki haijawa kubwa na kuwa inatokana na ugeni wa mashindano hayo.

"Bingwa atajinyakulia kitita cha shilingi milioni tano, lakini kidhamu yake ikiwa ndogo tutamkata kutoka milioni tano mpaka milioni tatu, hiyo tumeviambia vilabu vyote vinatambua hilo, lengo kuu ni kudumisha nidhamu kwa timu," alisema Salumu.

Alimalizia kwa kuwaomba wadau kujitokeza kwa wingi kushuhudia michuano hiyo katika vituo husika, kwani huwepo wake unalenga kuinua, kuendeleza na kudumisha mahusiano katika familia ya wanamichezo.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items