Mkuu wa Benki Kuu ya Ulaya Christine Lagarde ametoa wito wa kuidhinishwa bila kuchelewa mfuko wa Umoja wa Ulaya wa fedha za kuuokoa uchumi ulioharibiwa na janga la virusi vya Corona. Hii ni baada ya Poland na Hungary kutumia kura zao za turufu kuipinga bejeti hiyo.
Akizungumza kabla ya kuanza mazungumzo muhimu ya viongozi wa Umoja wa Ulaya kuhusu mgogoro huo, Lagarde amesema fedha zaidi za mpango huo unaweza kurahisisha utekelezwaji wa sera za bajeti, na hasa katika eneo la nchi zinazotumia sarafu ya euro, ambalo lina nafasi ndogo ya kifedha.
Viongozi wa Ulaya watajadili leo mjini Brussels mpango huo wa kifedha wa euro trilioni 1.8, lakini maafisa hawatarajii kupatikana suluhisho wiki hii.
