F Hii ndio ratiba ya hatua ya 16 Ligi ya Mabingwa Ulaya | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Hii ndio ratiba ya hatua ya 16 Ligi ya Mabingwa Ulaya

Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA), mchana leo Desemba 14, 2020, limeweka wazi droo ya hatua ya 16 bora ya michuano ya klabu bingwa barani humo, ambapo mabingwa wa kihistoria, klabu ya Real Madrid wamepangwa kucheza dhidi ya Atalanta ya nchini Italia.

Mabingwa watetezi wa michuano hiyo klabu ya Bayern Munich, imepangwa kuanza kucheza ugenini dhidi ya Lazio ya Italia Ilihali miamba ya soka ya Uhispania klabu ya Barcelona, uso kwa uso na PSG, miamba ya soka kutoka nchini Ufaransa ikiwa ni vita ya Messi dhidi ya Neymar Junior.

Borussia Monchengladbach ya Ujerumani kuvaana na Manchester City ya Uingereza, vijana watukutu wa Diego Simeone Atletico Madrid ya Uhispania watavaana na Chelsea ya Uingereza chini ya Kocha Frank Lampard.

Dortmund ya Ujerumani watasafiri hadi nchini Uhispania kuwafuata klabu ya Sevilla, wakati RB Leipzig ya Ujerumani wataumana na Liverpool ya Uingereza, FC Porto ya Ureno dhidi ya Juventus ya Italia ya CR7.

Michezo ya hatu ya 16 bora inatazamiwa kuanza kuchezwa tarehe 15 na 16 hadi tarehe 23 na 24 mwezi Februari, kwa michezo ya mzunguko wa kwanza na michezo ya marudiano kuchezwa tarehe 9 na 10 hadi tarehe 16 na 17 mwezi machi mwaka 2021.

 Monchengladbachi v Manchester City.

Lazio v Bayern

Atletico v Chelsea

Leipzing v Liverpool

Porto v Juventus

Barcelona v PSG

Sevilla v Dortmund

Atlanta v Real Madrid

Post a Comment

0 Comments