Na Faruku Ngonyani, Mtwara
Wakulima Mkoani Mtwara wametakiwa kujikita Zaidi kwenye kilimo ili waweze kujikwamua na kuongeza uchumi hapa nchini.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byanwa kwenye muendelezo wa ziara yake aliyofanya Wilaya ya Masasi ya “Ondoa mapori Ongeza uzalishaji”ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa wakulima namna ya kuongeza uzalishaji katika mazao mbalimbali yanaolimwa wilani humo.
Alipokuwa katika kijiji cha Chingululu kata ya Namatutwe Mkuu wa Mkoa alifanya mkutano na wakulima shambani akiwa ameambatana na Dr.Kapinga mtaalam wa kilimo kutoka Taasisi ya utafiti wa kilimo TARI Naliendele ambapo alitoa elimu namna ya kupogelea mikorosho lakini kuondoa mikorosho ya mda mrefu na kuwaelekeza kupanda mikorosho mipya ili zao hilo liweze kuongezeka uzalishaji wake.
Akiwa katika kijiji hiko Mkuu wa Mkoa amewaeleza wakulima kwa sasa Tanzani imefikia uchumi wa kati lakini pia amesisitiza kwa sasa inaweza kufikia uchumi wa juu endapo wakulima watazingalia kilimo bora katika uzalishai wake.
Mkuu wa Mkoa Gelasius byankwa amemaliza ziara yake ya kuhamasisha na kutoa elimu kwa wakulima namna ya kuongeza uzalishaji kwenye kilimo huku akiwataka wakulima hao kuzingatia maelekezo aliyoyatoa ili waweze kuongeza uzalishaji wake.
Mkuu huyo wa Mkoa ameongeza kuwa Ifikapo tarehe moja Februari 2021 mkulima yeyote atakaebainika amesafisha shamba kwa kuchoma moto atapigwa faini elfu hamsini,vijana wasiokuwa na mashamba watapigwa faini elfu hamsini na atakaebainika ametelekeza shamba pia atapigwa faini ya shilingi elfu hamsini.
Wilaya ya Masasi uzalishaji wa zao la korosho umeshuka kwa misimu mitatu mfululizo huku zao la ufuta likiendelea kufanya vizuri.

0 Maoni