Ronaldo afikisha jumla ya mabao 750 kwenye soka


 Bao lililofungwa jana na Cristiano katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Dynamo Kyiv, limemfanya kufikisha jumla ya mabao 750 katika maisha yake ya soka. Ronaldo amefunga mabao hayo akiwa Manchester United, Real Madrid, timu ya Taifa Ureno, Sporting Lisbon na Juventus.

Katika mchezo huo, #Ronaldo alifunga  bao hilo dakika 53, baada ya usajili wa mkopo Federico Chiesa kufunga bao lake la kwanzakwa kichwa akitumia krosi ya Alex Sandro. Baada ya Ronaldo kuongeza la pili, Morata aliifunga 3-0 na kuwa bao lake la sita la Ligi ya Mabingwa msimu huu.

Katika michezo jumla ya michezo yake, #Ronaldo alifunga mabao matano akiwa na Sporting Lisbon, mabao 450 katika michezo 292 akiwa na Real Madrid na mabao 118 akiwa na Manchester United na mabao 102 kwa timu ya Taifa ya Ureno na mengine 75 akiwa na Juventus.


Post a Comment

0 Comments