Bach asema IOC imedhamiria kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Tokyo


Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki - IOC Thomas Bach amesema maafisa wa Japan wamedhamiria kuandaa mwaka huu

 Michezo ya Olimpiki ya Tokyo yenye mafanikio na salama, akipuuzilia mbali uvumi wa kuwa tamasha hilo maarufu litafutwa.

 Lakini Bach amekiri kwa mara ya kwanza kuwa mashabiki huenda wasiruhusiwe kuhudhuria. Baada ya kuwepo kwa mjadala kuhusu uwezekano wa kuandaliwa Michezo hiyo ya 2020, ambayo tayari iliahirishwa kwa mwaka mmoja hadi Julai 23, Bach ametoa wito wa kuwepo na subira na kusema kuwa IOC imelenga kikamilifu katika kuandaa tamasha hilo wakati huu wa janga la virusi vya corona. 

Akizungumza na wanahabari kwa njia njia ya video, Bach amesema changamoto za kuandaa mashindano hayo zimekuwa ngumu hata zaidi kutokana na janga hilo la kiafya, lakini kuna hatua zinazotayarishwa ili kuyafanikisha katika mazingira ya sasa.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi