Bill Gates, Soros na Rockefeller walaumiwa kwa Covid-19

 


Mahakama ya Peru imemshtaki mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates, na mfanyabiashara wa Marekani George Soros na familia ya kitajiri ya Rockefeller kwa madai ya kutengeneza virusi vya corona (Covid-19).


Madai ya kwamba virusi vya corona vilivyoathiri dunia nzima, vimetengezwa katika mazingira ya maabara yameibuka tena.


Mahakama ya Peru imechukua uamuzi wa kuanzisha uchunguzi juu ya jinsi mlipuko wa janga la coronavirus ulivyoanza na kuenea.


Mahakama hiyo ilisema kwamba Covid-19 ni kosa la Bill Gates, George Soros na Rockefeller, wakidai kwamba limetoka mikono mwa matajiri.


Kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya Urusi, iliandikwa "Hakuna serikali ya ulimwengu, watu halisi na wa kisheria, isipokuwa Bill Gates, Soros, Rockefeller, walioweza kudai kuwa janga hili linatabirika."


Baada ya uchunguzi huu kufichua taarifa hizi na kusambazwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, Mahakama ya Peru pia iliachukua uamuzi kuingilia uchunguzi.


Katika taarifa iliyotolewa, ilisemekana kwamba uchunguzi wa awali ulifunguliwa kufuatia uamuzi wa majaji waliosaini.


Lengo kuu la majadiliano haya ni muungano wa chanjo ulimwenguni wa wakfu wa Bill & Melinda Gates Foundation, ulioanzishwa na Bill Gates pamoja na mkewe.


Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii walikuwa wakimlaumu Bill Gates. Wakati kuna nadharia nyingi za njama zinazoenea kwenye tovuti, Bill Gates alikuwa mlengwa kwa kudaiwa kutengeneza chanjo ya corona ili kufuatilia mabilioni ya watu kupitia 'mcrochips.'


Post a Comment

0 Comments