LATRA: Mfumo wa tiketi za kielektroniki haulengi kuumiza yeyote

 


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Usafiri Ardhini (LATRA), Gilliard Ngewe amesema uamuzi wa mabadiliko ya mfumo wa kawaida wa kukata tiketi hauna lengo ya kuumiza upande wowote

Kukata tiketi kielektroniki kutawezesha Sekta ya Uchukuzi kukua na kuondoa usumbufu ambao umekuwa ukijitokeza kwa wanaosafiri kwani baadhi yao wamekuwa wakikatiwa tiketi zisizo halali

Amefafanua, tiketi ya kawaida inapokatwa, fedha hupita kwa watu wengi na kinachomfikia Msafirishaji ni kidogo, hali inayopelekea wapate hasara na washindwe kulipa Kodi

Mfumo huo unalenga kusaidia kila upande na Serikali ipo tayari kukaa na Wamiliki wa Mabasi ili kuboresha sekta hiyo


Post a Comment

0 Comments