Marekani kufungua ubalozi mdogo Sahara Magharibi


Marekani imeanza mchakato wa kufungua ubalozi wake mdogo katika eneo linalozozaniwa la Sahara Magharibi.

 Hii inajiri kufuatia hatua ya Marekani kutambua mamlaka ya Morocco juu ya eneo hilo kama jibu la kujali masilahi baada ya Morocco kurejesha uhusiano wake na Israel. 

Balozi wa Marekani nchini Morocco David Fischer alitembelea bandari ya Dakhla iliyoko eneo inayozozaniwa lakini inayodhibitiwa na Morocco maili 895 kusini magharibi mwa Rabat, kuashiria mwanzo wa juhudi za kufungua ofisi ya kidiplomasia. 

Morocco inadhibiti sehemu kubwa ya Sahara Magharibi ambayo ni koloni la zamani la Uhispania lakini imezozaniwa tangu miaka ya 1970, na chama cha Polisario Front kinachotaka eneo hilo kuwa huru.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi