Wadhifa mpya kwa kiongozi wa Korea Kusini


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, amepewa wadhfa mpya wa kuwa katibu mkuu wa chama tawala cha Korea Workers Party.

Kulingana na taarifa za Shirika la Habari la Korea (KCNA), katika kikao cha 6 cha Bunge la 8 la Chama cha Korea Workers Party, kilichofanyika hapo jana katika mji mkuu Pyongyang baada ya mapumziko ya miaka 5, wadhfa wa mwenyekiti wa chama ambao hapo awali ulikuwa na baba yake Kim Jong-il na babu yake Kim Il-sung, ulibadilishwa na kuwa katibu mkuu wa chama na kukabidhiwa Kim Jong-un.

Imeelezwa kwamba Chama cha Korea Workers Party kimemkabidhi Kim wadhfa huo kwa lengo la kuimarisha mamlaka yake.

Wakati huo huo, jeshi la Korea Kusini limetangaza kuwa limepata taarifa za kijasusi ambazo zinaonyesha Korea Kaskazini inafanya gwaride la kijeshi katika eneo la Pyongyang Square usiku wa Jumapili.

Ofisi ya Idara Kuu ya Huduma za Umma nchini Korea Kusini iliripoti kuendeleza uchunguzi endapo gwaride hilo lilikuwa la kweli au mazoezi.

Waangalizi wanadai kwamba gwaride hilo linaonekana kuwa na mifumo mipya ya silaha za kuonyesha nguvu dhidi ya utawala wa Joe Biden nchini Marekani.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alitangaza orodha ya mifumo ya teknolojia ya hali ya juu inayoendelea waliyobainisha katika vikao vya awali na kutishia uimarishaji wa silaha za nyuklia.

Katika hotuba yake, kiongozi huyo wa Korea Kaskazini alisisitiza kuwa Marekani ni "adui mkuu" wa nchi hiyo na "yeyote atakayechukua madaraka nchini Marekani hatabadilisha muundo wa kimsingi na sera ya uhasama."

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi