Waziri Mkuu wa zamani wa Kyrgyzstan, Sadir Caparov ameshinda uchaguzi wa urais kwa asilimia 79.18 ya kura, kwa mujibu wa matokeo yasiyokuwa rasmi.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na Baraza la Kura ya Maoni Nurjan Shaildabekova, alisema kuwa taratibu za kupiga kura zilikamilishwa kwenye vituo 2,474 na asilimia 96.44 ya kura zimehesabiwa.
Akibainisha wapigaji kura 3,563,574 walijiandikisha kwenye uchaguzi huo, Shaildabekova alisema kuwa wapigaji kura 1,339,638 walijitokeza kutekeleza zoezi hilo amabo wanajumuisha asilimia 37.59.
Shaildabekova pia alichapisha taarifa inayoashiria Sadır Caparov kuongoza kwa asilimia 79.18 ya kura kwa mujibu wa matokeo yasiyokuwa rasmi.
Shaildabekova aliongezea kusema kuwa asilimia 34.29 ya wapiga kura walishiriki kura ya maoni kwa wakati mmoja ambapo asilimia 81.2 kati yao walipiga kura ya rais.
