Marekani kujiunga na mpango wa chanjo wa COVAX

 


Marekani imetangaza leo kuwa inajiunga na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kutoa chanjo ya virusi vya corona kwa usawa kati ya mataifa tajiri na masikini duniani. 

Mshauri mkuu wa masuala ya afya nchini humo Anthony Fauci, amesema baadae leo rais Joe Biden atatia saini amri ya kuwezesha Marekani kuwa sehemu ya mpango huo unaofahamika kama COVAX. 

Tangazo hilo linakuja saa chache tangu rais Biden alipositisha hatua ya mtangulizi wake Donald Trump ya kuitoka Marekani kutoka Shirika la Afya duniani WHO. 

Wakati huo huo utawala wa Biden leo umetangaza mpango wa taifa wa kukabiliana na janga la virusi vya corona wa dola Trilioni 1.9 unaojumisha matumizi kwa ajili ya chanjo na upimaji wa COVID-19.


Post a Comment

0 Comments