Merkel atetea vikwazo vya kupambana na COVID-19

 


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel leo ametetea uamuzi wa kurefusha muda wa kufungwa kwa shughuli za umma nchini mwake hadi katikati ya mwezi unaokuja, akisema ni muhimu kwenye kupunguza kasi ya kusambaa kwa aina mpya kirusi kipya cha corona. 

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi habari, Merkel amesema wakati vizuizi vilivyowekwa vinaonesha kupunguza kiwango cha maambukizi, litakuwa kosa kubwa kulegeza masharti hayo hivi sasa nchini Ujerumani. 

Merkel amesema ugunduzi unaonesha aina mpya ya kirusi cha corona inaambukiza zaidi kuliko ile ya awali, na ndiyo sababu kuu ya kuongezeka kwa kasi kwa mambukizi COVID-19 nchini Uingereza. 

Ujerumani ambayo imekuwa chini ya vizuizi tangu mwezi Novemba, imeripoti zaidi ya vifo1,000 na mambukizi mapya zaidi ya 20,000 katika muda wa saa 24 zilizopita.


Post a Comment

0 Comments