Jan 11, 2021

Tetesi za soka kimataifa


 Napoli wameamua kumfanya mlinzi wa Arsenal Mskochi Kieran Tierney lengo lao la muda mrefu baada ya kumkosa nyota huyo aliye na umri wa miaka 23 mwanzo wa msimu huu. (Telegraph - subscription required)

Manchester United inajiandaa kumenyana na Paris St-Germain katika mbio za kumsaka kiungo wa kati wa Brest na Ufaransa mwenye chini ya miaka 21 Romain Faivre. (Sun)

Everton wanatafakari uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati Mbrazil Felipe Anderson, 27, ambaye yuko Porto kwa mkopo kutoka West Ham United. (Teamtalk)

Chelsea hawako tayari kumuachilia kiungo wa kati wa England Ross Barkley kujiunga na Aston Villa - ambako anacheza kwa mkopo wa msimu mzima -huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 akisalia na miaka miwili na nusu kwenye mkataba wake. (Birmingham Mail)

Mshambuliaji wa Uhispania Brahim Diaz anajiandaa kuondoka AC Milan kurejea Real Madrid mkataba wake wa mkopo utakapokamilika, japo klabu hiyo ya Italia inataka kusalia na nyota huyo aliye na umri wa miaka 21. (Le10Sport - in French)

Newcastle United huenda isiwe maskani mapya kwa mlinzi wa Chelsea Muingereza Fikayo Tomori, 23 ambaye anajiandaa kuondoka mwezi huu. (Chronicle)

Winga wa England Jadon Sancho amekiri kwabma amekuwa na msimu mgumu Borussia Dortmund tangu alipohusishwa na tetesi za kujiunga na Manchester United, lakini nyota huyo wa miaka 20- anaamini kuwa amerejelea hali yake ya kawaida. (Manchester Evening News)

Wakala wa kiungo wa kati wa Manchester City Fernandinho amegusia uwezekano wa mchezaji huyo aliye na umri wa miaka 35- kurejea klabu ya Brazil ya Athletico Paranaense mkataba wake na City utakapomalizika. (Globo Esporte - in Portuguese)

Fenerbahce wanataka kumnunua kiungo wa kati wa Mturuki Ozan Tufan ,25, kwa £14m huku Crystal Palace, West Bromwich Albion na CSKA Moscow ya Urusi pia zikimng'ang'ania mchezji huyo. (Hurriyet - in Turkish)

Liverpool imefanya mazungumzo na klabu za Ubelgiji, Ujerumani na Uswizi kuhusu uwezekano wa kumsajili kwa mkopo mlinzi wa Uholanzi wa miaka 19 Sepp van den Berg. (Goal)

Mshambuliaji wa Southampton Dan N'Lundulu, 21, ambaye aliiwakilisha England katika kiwango cha vijana, ananyatiwa na Real Betis. Kiungo huyo amesalia na miezi 18 katika mkataba wake wa sasa. (TodoFichajes - in Spanish)

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger