Watu wenye ulemavu Manyara wapatiwa elimu ya kupambana na Rushwa


 Na John Walter-Manyara

Watu Wenye Ulemavu wa kutokusikia mkoani Manyara wamepatiwa mafunzo ya kupambana na Rushwa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Manyara ili waweze kushirikiki katika vita hivyo.

Wakizungumza katika kikao kazi  cha Cha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa pamoja na chama cha watu wenye ulemavu wa kutokusikia (CHAVITA), katibu wa CHAVITA mkoa wa Manyara Anna Ngalawa ameeleza kuwa mawasiliano ni changamoto kubwa kwa viziwi katika maendeleo.

Ngalawa amesema matarajio yao makubwa ni Viziwi kujua wapi pa kuelekea kuripoti pindi wanapokutana na changamoto mbalimbali katika ofisi za serikali au watu binafsi.

Kwa upande mwingine watu wenye ulemavu wa kutokusikia mkoani hapa,  wamelalamikia rushwa ya ngono katika ofisi mbalimbali wanapokwenda kuomba ajira suala linalochangia kuzotesha maendeleo yao.

Amemuomba mkuu wa mkoa wa Manyara  kuwasaidia kupata ofisi ambayo itawawezesha kufika na kutoa malalamiko waliyonayo.

Mkuu Wa Takukuru Mkoa Wa Manyara Holle Makungu akitoa semina hiyo kwa kundi hilo lenye  ulemavu katika ukumbi wa mikutano wa TAKUKURU, amewataka watu wenye ulemavu kushiriki katika vita dhidi ya Rushwa kwa kutoa taarifa ili hatua ziweze kuchukuliwa.

Mkuu Wa Mkoa Wa Manyara Joseph Mkirikiti amesema watu wenye Ulemavu wanapaswa kuhudumiwa vizuri na kuwekewa wakalimani katika huduma zote za Jamii.

Post a Comment

0 Comments