Biden asema Trump ana tabia zisizo za kawaida

 


Rais wa Marekani Joe Biden amemwambia Rais wa zamani Donald Trump kuwa hatapewa ripoti za taarifa za siri kwa sababu ya "tabia yake isiyo ya kawaida".


Akizungumza na CBS, Biden, amesema,


"Sidhani anahitaji kupewa taarifa nyeti. Je! Hiyo ni faida gani?".


Akisisitiza kuwa Trump alikuwa na "tabia isiyo ya kawaida", Biden alidai kwamba Trump hawezi kuaminiwa kutunza siri ya habari nyeti.


Nchini Marekani, marais wana utamaduni wa kuendelea kupata taarifa nyeti za kiintelijensia hata baada ya kipindi chao cha kazi.


Kulingana na New York Times, Trump hatapewa fursa hiyo kwa mara ya kwanza katika historia ya Marekani.


Trump alikosolewa kwa kuvunja utamaduni katika mchakato wa kuachiakiti cha urais kwa kutomsubiri Biden, ambaye alishinda uchaguzi wa urais mnamo Novemba 3, 2020.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items