Biden kutoa tamko kuhusu Saudi Arabia siku ya Jumatatu


Rais wa Marekani Joe Biden amesema serikali yake itatoa tamko juu ya Saudi Arabia kesho Jumatatu kufuatia ripoti ya kijasusi ya Marekani kusema kuwa mrithi wa kiti cha ufalme wa taifa hilo Mohammed Bin Salman aliamuru mauaji ya muandishi habari Jamal Khashoggi. 


Utawala wa Biden umekosolewa hasa katika ripoti ya gazeti la Washington Post iliyosema Biden angeonesha nguvu zake kwa Mohammed Bin Salman ambaye hakuwekewa vikwazo vya aina yoyote licha ya kutajwa kuhusika na mauaji ya Khashoggi. 


Biden amesema atatangaza Jumatatu hatua watakayochukua kwa Saudi Arabia. Jamal Khashoggi aliyekuwa uhamishoni Marekani akiandika ripoti zinazomkosoa Mohammed Salman na serikali ya Saudi Arabia, aliuwawa tarehe 2 mwezi Oktoba mwaka 2018, katika ubalozi wa Saudi Arabia mjini Istanbul, Uturuki.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items