EU kuiwekea vikwazo vipya Urusi

 


Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya (EU) kuhusu Maswala ya Kigeni na Sera ya Usalama Joseph Borell amesema kuwa Urusi haitaki kufaidika na mazungumzo ya kujenga uhusiano na EU na kuashiria uwezekano wa kuweka vikwazo vipya dhidi ya nchi hii.


Josep Borell, katika taarifa yake kuhusu ziara yake huko Moscow mnamo Februari 4-6, amesema kwamba alijadili uhusiano "wa wasiwasi" wa EU na Urusi, hasa baada ya kukamatwa kwa mpinzani wa Kremlin Alexey Navalny na kutokea kwa maandamano, mambo yanayofanya hali izidi kuwa mbaya.


Akikumbushia kwamba alitaka kujadili uhusiano unaozorota wakati wa ziara yake kabla ya Mkutano wa EU utakaofanyika Machi, Borrell aliongeza kwa kusema,


"Mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika kwa fujo na uamuzi wa kuwafukuza wanadiplomasia 3 kutoka nchi za EU wakati wa ziara yangu ulionyesha kuwa mamlaka ya Urusi haitaki kuchukua fursa ya mazungumzo yenye kujenga zaidi na EU. Hii haikutarajiwa, na inasikitisha. "


Borrell amebainisha  kwamba EU na Urusi hazingeweza kukubaliana juu ya maswala mengi kama vile Belarusi, Ukraine, Georgia, Syria na Libya.


Akisisitiza kuwa watajadili uhusiano na Urusi katika mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa EU mnamo 22 Februari, Borrell alisema.


"Kama kawaida, nchi wanachama zitaamua hatua za kuchukuliwa, na hizi zinaweza kujumuisha vikwazo." 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi