Maelfu ya raia wa Myanmar wameandamana leo kwenye mitaa ya mji mkuu wa zamani Yangon kulaani mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa mwanzoni mwa wiki na kushinikiza kuachiwa huru kwa kiongozi wa kiraia Aung San Suu Kyi.
Licha ya utawala wa kijeshi kuzuia mtandao wa intaneti wanaandamanaji wenye hasira walijitokeza kwa wingi wakipaza sauti huku wakiwa na mabango yenye maandishi yanayopinga kile kinachotjwa kuwa "udikteta wa kijeshi" Wengi ya waliohudhuria walivalia mavazi mekundu ambayo ni rangi ya chama cha NLD kinachoongozwa na Suu Kyi kilichoshinda kwa wingi mkubwa wa kura uchaguzi mkuu wa Novemba 8 mwaka uliopita, matokeo yanayopingwa na majenerali wa jeshi.
Mapema jana utawala wa kijeshi uliamuru kufungwa kwa muda mitandao ya kijamii ya Twitter na Istagram baada ya kufanya hivyo pia kwa mtandao wa Facebook wakisema inatumika kuvuruga uthabiti wa taifa hilo.