Marekani yawaonya Wahouthi baada ya kuwatoa orodha ya magaidi


Utawala wa Biden nchini Marekani jana umetoa onyo kwa waasi wa Kihouthi nchini Yemeni, dhidi ya kuwashambulia raia, saa chache baada ya kuliondoa kundi hilo kwenye orodha ya makundi ya kigaidi. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani pia imelitaka kundi hilo kusitisha operesheni mpya za kijeshi nchini Yemen. 


Dai hilo limekuja siku bili tu baada ya utawala kulifahamisha bunge kwamba utawaondoa Wahouthi kutoka orodha ya mataifa ya kigaidi ya kigeni, uorodheshaji unaofuatana na vikwazo vikali vya Marekani. Pia limekuja siku tatu baada ya rais Joe Biden kuamuru kukomeshwa kwa msaada kwa operesheni za kijeshi zinazoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya waasi hao. 


Kuondolewa kwa Wahouthi kwenye orodha ya masharika ya kigaidi kumesifiwa na mashirika ya misaada, yalioukosa utawala wa Donald Trump kwa kuliorodhesha kundi hilo katika siku zake za mwisho, yakisema hatua hiyo ingechochea kile ambacho Umoja wa Mataifa unakiita mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu, kwa kuzuwia usafirishaji wa mahitaji kwa raia walioko katika hatari ya kukumbwa na baa la njaa.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi