Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini mkoa wa Manyara Mheshimiwa Daniel Sillo ameahidi kutoa mashine kwa ajili ya kufanya machapisho na kutoa nakala katika shule ya Sekondari Maganjwa na Dabil ili kuwaondolea usumbufu wanaoupata kwenda mbali kuchapisha mitihani.
Amesema mashine hizo zitawaondolea usumbufu walimu,wanafunzi pamoja na wazazi ambao hulazimika kugharamia uchapishwaji wa mitihani kwa watoto wao.
Sillo amewaambia wananchi wa Kata hiyo kuwa hadi kufika mwezi wa sita mwaka huu atakuwa tayari ameshazinunua mashine hizo (PRINTERS) mbili mpya kwa kutumia mshahara wake.
Ametoa ahadi hiyo wakati alipofanya ziara katika kata ya Dabil ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo kuhamasisha wananchi wafanye kazi kama anavyosisitiza Rais John Magufuli na kutoa shukrani kwa kumuamini kuwa mwakilishi wao Bungeni.
Katika hatua nyingine Sillo amesema ataendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Jimbo hilo.
0 Comments