Mgombea wa chama tawala Niger aongoza matokeo ya awali


Mgombea wa chama tawala nchini Niger Mohamed Bazoum ameimarisha uongozi dhidi ya mpinzani wake wakati shughuli ya kuhesabu kura ikiendelea kufuatia duru ya pili ya uchaguzi wa rais katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

 Huku kura za vituo 196 kati ya 266 zikiwa zimehesabiwa, matokeo ya mwanzo yanaonyesha waziri wa zamani wa mambo ya ndani Bazoum akiwa kifua mbele dhidi ya mpinzani wake, rais wa zamani Mahamane Ousmane, akiwa na karibu asilimia 52.9 ya kura. 

Duru ya pili ya uchaguzi huo inayolenga kushuhudia kwa mara ya kwanza katika historia ya Niger makabidhiano ya madaraka kutoka kwa rais mmoja aliyechaguliwa kidemokrasia hadi kwa mwingine, iliandaliwa Jumapili baada ya kukosekana mshindi wa moja kwa moja katika duru ya kwanza Desemba mwaka jana.

Post a Comment

0 Comments