Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amekana makosa ya rushwa mahakamani leo, baada ya kuanza tena kwa kesi yake, wiki sita kabla ya wapiga kura kurudi tena vituoni kuamua juu ya uongozi wake wa miaka 12.
Netanyahu alishtakiwa mwaka uliopita kwa udanganyifu, kuvunja uaminifu na kupokea hongo katika kesi tatu tofauti.
Katika miezi ya karibuni, Waisrael wamekuwa wakifanya maandamano ya kila wiki wakimshinikiza ajiuzulu na kuikosoa serikali yake kwa namna ilivyoshughulikia janga la virusi vya corona.
Netanyahu amethibisha mahakamani kwamba majibu ya maandishi yaliowasilishwa mahakamani yalikuwa jibu lake kwa mashtaka yanayomkabili. Hii ndiyo ilikuwa mara ya pili kwa Netanyahu kufika mahakamani kuhusiana na mashtaka hayo.
MAra ya kwanza ilikuwa mwezi Mei mwaka jana, wakati aliposomewa mashtaka kwa mara ya kwanza.
