Polisi Moshi wamsaka aliyetelekeza gari lililopakia mirungi


 Polisi  Mkoa wa Kilimanjaro wanamsaka, Gilbert Weche kwa madai kuwakimbia polisi baada ya kutelekeza gari lililokutwa na mirungi kilo 166.5.


Kaimu Kamanda wa polisi wa Mkoa huo, Ronald Makona ameeleza hayo leo Jumamosi Februari 6, 2021  wakati jeshi hilo likiwa kwenye operesheni  ya kukamata dawa za kulevya.


Amesema Februari 4, 2021 saa 7:45 mchana polisi wakiwa kwenye doria katika barabara ya Himo-Moshi,  walilitilia shaka gari lililokuwa likiendeshwa na Weche aina ya Toyota Corolla na walipomsimamisha hakusimama.


Amebainisha waliifuatilia kwa nyuma na  mtuhumiwa huyo alipofika barabara ya Kawawa alilitelekeza gari hilo katika mashamba na kukimbia.


"Polisi walipokagua gari walikuta mirungi kilo 166.5 iliyokuwa imefungwa kwenye mifuko ya plastiki,” amesema kamanda huyo akibainisha kuwa gari hilo linashikiliwa na polisi.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items