Utawala wa kijeshi Myanmar waamuru kufungwa kwa Twitter na Instagram

 


Utawala wa kijeshi nchini Myanmar umeziamuru kampuni za mawasiliano nchini humo kuifunga kwa muda mitandao ya kijamii ya Twitter na Istagram siku chache tangu ilipoweka vizuizi kama hivyo kwa mtandao wa Facebook. 


Kulingana na tovuti moja ya habari Jeshi limezitaka kampuni za simu kuzuia upatikanaji wa mitandaoni hiyo kuanzia usiku wa kuamkia leo ikisema inatumika kuvuruga uthabiti wa taifa hilo. 


Amri hiyo kutoka wizara ya uchukuzi na mawasiliano imetolewa katika wakati hasira ya umma inaongezeka tangu jeshi lilipofanya mapinduzi mapema siku ya Jumatatu na kuuondoa madarakani utawala wa kiraia. 


Miito ya kuitisha maandamano na kuwataka raia kutoutiii utawala wa kijeshi imendelea kusambaa mitandaoni tangu jehsi lilipowakamata viongozi wa serikali akiwemo kiongozi wa kiraia Aung San Suu Kyi katika uvamizi uliofanywa mapema wiki.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items