Profesa Mpangala afariki dunia

 


Profesa wa  Chuo Kikuu Katoliki Ruaha (Ruco) mkoani Iringa, Gaudence Mpangala amefariki dunia jijini Dodoma leo asubuhi Alhamisi Februari 4, 2021 baada ya kuugua ghafla.


Akizungumza na Mwananchi Digital leo mjukuu wa msomi huyo, Andrew Mpangala amesema, “babu alikuwa Dodoma kikazi lakini leo kati ya saa 2 na saa 3 asubuhi  akiwa katika safari kuelekea kwenye kikao alijisikia vibaya na kukimbizwa hospitali na ilivyofika saa tano akafariki dunia.”


Amesema mara ya mwisho kuwasiliana na babu yake ilikuwa jana na alimuagiza amtumie  taarifa mbalimbali alizotakiwa kuzifuata Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kisha azitume Dodoma.


“Leo asubuhi nikapiga simu yake akapokea dereva wake ambaye aliniambia babu hali yake sio nzuri na amekimbizwa hospitalini. Pia dereva akaniambia hakuna mtu wetu wa karibu Dodoma ili aende kumuangalia mzee,” amesema.


Profesa Mpangala  alikuwa mchambuzi wa  masuala mbalimbali hasa  ya siasa.


Andrew amesema mwili utapelekwa chuo cha Ruco kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho na baada ya hapo utapelekwa Dar es Salaam.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items