Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewaapisha Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria aliowateua hivi karibuni.
Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar walioapishwa ni Ibrahim Mzee Ibrahim na Haji Omar Haji ambao uteuzi wao ulianza tangu februari 1, 2021 na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria ambaye ni Khadija Shamte Mzee.
Majaji waliteuliwa tarehe 01 Februari 2021 na Rais wa Zanzibar na Dk. Hussein Ali Mwinyi chini ya Kifungu Namba 94 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 huku Khadija Shamte Mzee akiteuliwa na mnamo tarehe 07 Januari, 2021.
Viongozi hao wameapishwa katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Mwinyi Talib Haji.
