Ufaransa imesema inazungumza na serikali ya Ujerumani kujaribu kuepusha mipango ya vizuizi vya usafiri vilivyotangazwa na Ujerumani baada ya wasiwasi wa kusambaa kwa ugonjwa wa COVID 19 katika eneo la ufaransa la Moselle.
Taasisi ya kuzuwia na kudhibiti magonjwa nchini Ujerumani ya Robert Koch leo imeiorodhesha Moselle kuwa eneo la uangalizi baada ya kirusi kipya cha corona kilichogundulika kwa mara ya kwanza Afrika Kusini kuongezeka katika wilaya hiyo.
Hatua hiyo iliifanya serikali ya Ujerumani kutangaza kuwa itaweka vizuizi vya kusafiri kutoka eneo hilo kuingia Ujerumani kuanzia siku ya Jumanne.
Usafiri wa umma kati ya Moselle na majimbo mawili ya Ujerumani ya Rhineland na Saarland utasitishwa kwa muda na wale watakaofika huko kwa kutumia magari binafsi inabidi wawe na vyeti vya kuonesha hawana virusi vya corona.
