Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe amesema kwa sasa idadi ya wanawake ni kubwa mno katika uwekezaji wa viwanda hivyo, kuwataka wengine ambao hawajajisajili kukamilisha baadhi ya taratibu ili watambulike rasmi katika sekta hiyo.
Rai hiyo ameitoa wakati akizindua maonyesho ya Wikiya Viwanda ya Wanawake katika viwanja vya Posta Kijitonyama Manispaa ya Kinondoni yakitarajiwa kuhitimishwa Machi 8, siku ambayo ndiyo kilele cha siku ya Wanawake Duniani.
