Wanamgambo washambulia Mashariki mwa Congo na kusababisha vifo 10

 


Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limesema wapiganaji wanaoshukiwa kutoka kundi la waasi wa ADF, wamewaua watu 10 katika mashambulio mawili usiku wa kuamkia leo Kaskazini mwa nchi hiyo. 


Msemaji wa jeshi Luteni Jules Ngongo amesema waasi hao wamewaua kwa kuwakata vichwa watu wanane, katika kijiji cha Boyo Kaskazini Mashariki mwa mkoa wa Ituri, na baadae kuwapiga risasi na kuwaua watu wengine wawili katika eneo la Kainama. 


Luteni Ngongo amesema wanajeshi wake bado wanaendelea kuwatafuta washambuliaji. Maafisa wa maeneo hayo mawili wamethibitisha matukio hayo na kuongeza kuwa nyumba kadhaa pia zilichomwa moto. 


Wanamgambo wa ADF wanaoaminika kutokea Uganda walikita kambi Mashariki mwa Congo tangu mwaka wa 1995, bado hawajashambulia nchini Uganda kwa miaka kadhaa lakini wamekuwa wakilaumiwa kwa mauaji ya zaidi ya wakaazi 800 mwaka uliopita katika machafuko yaliotokea katika mikoa yote miwili ya Kivu Kusini na Kivu Kaskazini.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items