Wakulima wa shamba la Kahawa JK Nge’reng’ere kunufaika na mashine ya kusukuma maji toka chanzo cha maji


Na Timothy Itembe Mara.

WAKULIMA wa shamba la JK Nge’reng’ere wilayani Tarime mkoani Mara kunufaika na mashine ya kusukuma maji kutoka kilipo chanzo cha maji hadi  kwenye mashamba ya kahawa.

Wakulima hao watanufaika na mashine hiyo kutokana na ombi walilotoa mbele ya mkuu wa wilaya Tarime Mtemi Msafiri yeye pamoja na  msafara wake uliokuwa ukiongozwa na katibu tawala wa mkoa Mara,Karolina Mthapula wakati wa ziara ya wadau wa kahawa walipotembelea shambani hapo na kubainishiwa changamoto zilizopo.

Akisoma risala kwa mgeni rasimi kaimu kamanda kikosi 822 UJ,Luteni Kanali Gaudencea Joseph Mapunda alisema kuwa wanachangamoto ya mashine ya kusukuma maji kutoka kwenye chanzo cha maji na kwenda kuliko mashamba ya kahawa.

Mapunda aliongeza kusema kuwa shambani kwao wamepanda miche ya kahawa zaidi ya alfu 52 ndani ya shamba lenye ekaei 52 na kuwa miche ya kahawa inahali nzuri.

Katika ziara hiyo mkulima Devd Hechei wa kata ya Mbogi alisema kuwa wakulima kwa ujumla wanakumbwa na changamoto ya kutotembelewa na maafisa kilimo mara kwa mara ajambo ambalo linasabisha baadhi ya wakulima kulima kilimo cha mazoea ambacho hakina tija.

Pia Hechei aliongeza kuwa yeye binafsi ananufaika na zao la kahawa lakini anakumbana na changamoto ya bei pamoja na kutokuwa na miundombinu ya barabara karibu ya shamba hali ambayo inachangia kuwepo na usumbufu wa kusafirisha kahawa kutoka shambani.

Mkuu wa wilaya Tarime ambaye kwa siku hiyo alikuwa mwenyekiti na mwenyeji wa ziara ya wadau wa kahawa,Mtemi msafiri alitumia nafasi hiyo kuwataka wakulima kuendelea kulima zao la kahawa kwa sababu serikali imeliteuwa kuwa zao la kimkakati.

Kwa upande wake Kajiru Kisenge aliwataka wakulima wa shamba la kahawa JK Ng’ereng’ere kuandika maombi maalumu kwenda  bodi ya kahawa Tanzania kwaajili ya kuomba fedha ya kununulia mashine hiyo nayeye atasimia.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi